TAMKO LA UTUME WA KANISA
Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kuwafanya watu wote wawe wanafunzi wa Yesu, kutangaza Injili ya milele katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12, na kuuandaa ulimwengu kwa marejeo ya Kristo yaliyo karibu.
UTEKELEZAJI WA UTUME WETU
Kwa kuongozwa na Biblia na Roho Mtakatifu, Waadventista wa Sabato hutekeleza utume huu kupitia maisha yanayoakisi alivyoishi Kristo, katika kuwasiliana, kufanya wanafunzi, kufundisha, kuponya, na kuhudumia.
NJOZI YA UTUME WETU
Kwa kupatana na mafunuo ya Biblia, Waadventista wa Sabato tunauona utume wetu ukifikia kilele katika mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.
TAMKO LA UTAMBULISHO NA UTEKELEZAJI WA UTUME WETU
UTAMBULISHO WETU
Kanisa la Waadventista wa Sabato linajitambua kuwa ni Kanisa la masalio la unabii wa Biblia wa siku za mwisho. Washiriki wa Kanisa hili, mmoja mmoja au kwa pamoja, huelewa jukumu lao maalumu kama mabalozi wa ufalme wa Mungu, na wajumbe wa marejeo ya Yesu Kristo yaliyo karibu. Waadventista Wasabato wamejiandikisha kama jeshi la wafanyakazi pamoja na Mungu katika utume wa kuurejesha ulimwengu kutoka katika nguvu na uwepo wa uovu, kama sehemu ya Pambano Kuu baina ya Kristo na Shetani. Kwa hiyo, kila hali ya maisha ya mshiriki wa Kanisa huathiriwa na kusadiki na kuamini kuwa tunaishi katika siku za mwisho za unabii wa Biblia na kwamba kurudi kwa Yesdu Kristo kuko karibu sana.Waadventista Wasabato wameitwa na Mungu kuishi katika ulimwengu huu.Kila tendo la maisha ya Mkristo hufanyika “katika jina la Yesu” na kutangaza ufalme wake.