Church Structure

UTANGULIZI WA MUUNDO WA SHIRIKA NA UONGOZI WA KANISA WAADVENTISTA WA SABATO.

Picha za Kibiblia za Kanisa
Kanisa la Waadventista Wasabato, kwanza kabisa, ni jumuiya ya kiroho ya watu ambao
wamemkubali Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Biblia inatumia mifano au picha nyingi
kueleza uhusiano kati ya Mungu na watu wake. Picha hizi, katika Agano la Kale na
Jipya, mara nyingi hutumika kama vielelezo vya Kanisa. Zinajumuisha zifuatazo:
Kondoo pamoja na mchungaji (Isaya 40:11, Zekaria 9:16, Luka 12:32, Yohana 10:14-16,
Matendo 20:29)
Mwili wa Kristo (Warumi 12: 5, 1 Wakorintho 12; 27, Waefeso 1:22, 23,Wakolosai 1:24 na 2:19)
Mzabibu na matawi (Yohana 15:5)
Kaya ya imani (Waefeso 2:19, 1Timotheo 3:15)
Familia ya Mungu (Kumbukumbu la Torati 14:2, Hosea 11:1, Yohana 1:12, Warumi 8:15, 2
Wakorintho 6:18, Wagalatia 4:5-6)
Watoto wa Mungu (Mathayo 5:9, Luka 20:36 ) , Warumi 8:16, 21 na 9:26, 1 Yohana 3:1-10
Kujenga ( Mathayo 16:18, 1 Wakorintho 3:10, Waefeso 2:21, 1 Petro 2:5 )
Bibi-arusi ( Isaya 62:5 ) , 2 Wakorintho 11:2, Ufunuo 19:7-9)