Adventist Beliefs

Waadventista wasabato huipokea Biblia kama kanuni yao pekee. Masomo yaliyoko hapa ni Imani za Msingi kama Waadventista Wasabato wanavyoziona zikidhihirika katika Maandiko Matakatifu. Imani hizi, kama zilivyoorodheshwa hapa, hufanya uelekevu wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho yaliyojengwa juu ya neno la Mungu kama lilivyo na sio nadharia au mawazo ya jinsi mwanadamu anavyofundisha. Karibu katika mfulizo wa masomo haya ya Biblia. Ni imani yetu kuwa yatakujenga kiroho na pia utawaalika watu wengine kutembelea tovuti hii ili nao pia waupate mbaraka huu ambao utawajenga na kutujenga sote. Ikumbukwe tu kwamba Biblia inafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili watu wote wampendao Mungu kwa nia ya dhati wawe kamili, naam wakamilishwe ili wapate kutenda kila jambo jema.

#1. Maandiko Matakatifu

“Maandiko Matakatifu, Agano la Kale na Agano Jipya, ni Maandiko ya Mungu yaliyoandikwa,
yaliyotolewa kwa kuvuviwa wanadamu watakatifu wa Mungu ambao walinena na kuandika kwa
kuongozwa na Roho Mtakatifu. Katika Neno hilo, Mungu amewapatia wanadamu ujuzi muhimu kwa
wokovu. Maandiko Matakatifu ni ufunuo usiokosea wa mapenzi yake Mungu. Ndicho kiwango cha tabia,
kipimo cha uzoefu, mfunuaji mwenye mamlaka wa mafundisho na kumbukumbu ya kuaminika ya
matendo ya Mungu katika historia.” (2Pet.1:20, 21; 2Tim.3:16, 17; Zab.119:105; Mith. 30:5, 6; Isa.8:20;
Yoh. 17:17; 1Thes. 2:13; Ebr.4:12)
Hakuna kitabu ambacho kimepata kupendwa, kuchukiwa, kuhofiwa, kushutumiwa kama Biblia. Watu
wamekufa kwa ajili ya Biblia. Wengine wameua kwa ajili yake. Imehamasisha matendo makubwa na ya
maana ya mwanadamu, na imelaumiwa kwa matendo maovu ya wanadamu. Vita vimepiganwa kwa ajili
ya Biblia, mapinduzi yamepangwa kwa kusoma kurasa zake, falme zimeangushwa kupitia fikra zake.
Watu wa kila namna, wanathiolojia kwa mabepari, mafashisti kwa wafuasi wa Karl Max, madikteta kwa
wakombozi, wapenda njia za amani kwa wapiganaji wa kivita, wote hujifunza maandiko kuhalalisha
matendo yao.
Tofauti ya Biblia, haitokani na kule kutokulingalishwa kwake na mivuto ya kisiasa, kiutamaduni, na kijamii
bali kutokana na jinsi ilivyo na inachofundisha. Ni ufunuo wa Mungu– Mtu pekee, Mwana wa Mungu,
Yesu Kristo, Mwokozi wa Ulimwengu

#2. Utatu Mtakatifu

Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa Nafsi tatu za milele. 

Mungu hafi, mwenye uwezo wote, anajua yote, juu ya yote, na yuko daima. 
Yeye hana kikomo na zaidi ya ufahamu wa mwanadamu, bado anajulikana kupitia ufunuo Wake binafsi. 


Mungu, ambaye ni upendo, anastahili daima kuabudiwa, kuabudiwa, na kuhudumiwa na viumbe vyote. 
0
( Mwa. 1:26; Kum. 6:4; Isa. 6:8; Mt. 28:19; Yoh. 3:16 ; 
 2 Kor. 1:21, 22; 13:14; Efe. 4:4-6 ) ; 1 Petro 1:2.)