Siku 10 za Maombi

Kurejea Madhabahuni

UJUMBE KUTOKA NTUC & STUM
Kwa waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato katika Northern Tanzania Union Conference na Southern Tanzania Union Mission, na nje ya Union hizi; tunawatakia Amani, Baraka na furaha, moyo wa kumpenda Mungu na  kumtumikia mnapopitia masomo haya ya ‘Siku kumi za maombi’ kwa mara nyingine tena.

Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyotulinda tangu Januari mwaka jana (2022) tulipokuwa na program hizi. Mungu wetu apewe sifa. Tunawakaribisha katika maombi ya mwaka huu tukishauri viongozi wa makanisa wahamasishe waumini kushiriki kikamilifu kila siku na kwa wakati katika program hizi bila kukosa, ili wote wahesabiwe katika wale watakaopokea mibaraka itakayoandamana na maombi haya. Kanisa mahalia lipange muda muafaka kadiri inavyowezekana, utakaowawezesha waumini wote pamoja na wageni kuhudhuria.
 
Ikiwezekana kila Conference au field ibuni namna ya kufanya juma hili liwe ni juma la pekee na la kuvutia. Ili kufanya program hii iwe na mguso mkubwa wa kiroho, tunashauri zoezi hili lifanyike kwa kubadilishana wahudumu kanisa moja na jingine au mtaa kwa mtaa. Ikiwa kuna visa vyovyote vinavyofunua jinsi Mungu alivyodhihirisha uwezo wake kwenye jumuiya ya waumini (kanisa) au kwa mtu mmoja mmoja katika siku hizi kumi za maombi, basi visa hivyo vitumwe Union kupitia kwa Makatibu wa Chama cha Wachungaji wa Conference mahalia ili viunganishwe na visa vya sehemu zingine duniani. Bwana awabariki mnapopitia masomo haya na kuyaweka katika uzoefu. Taarifa hizi zitufikie ndani ya mwezi wa January 2023.
 
Masomo haya yameandaliwa na Kitengo cha Uchungaji (Ministerial) – ‘Siku Kumi za Mombi’- cha Konferensi Kuu ya kanisa la Waadventista wa Sabato (GC) na kuhaririwa Katibu wa Chama cha Wachungaji wa NTUC, Mchungaji Davis Fue. Yametafsiriwa na Moseti Chacha wa kanisa la Waadventista wa Sabato la Lemara.
Ni mimi Mjoli wenu
Pastor Davis Fue
Simu: +255 764 151 340/655 151 340
Baruapepe: vugwasuji@gmai.com